,

Mbegu Quotes

Quotes tagged as "mbegu" Showing 1-8 of 8
Enock Maregesi
“Mbegu tunazopanda leo ni mazao ya msimu ujao. Ukipanda mbegu mbaya utavuna mabaya. Ukipanda mbegu nzuri utavuna mazuri. Ukitenda mabaya leo kesho yako itakuwa mbaya. Ukitenda mazuri leo kesho yako itakuwa nzuri. Okoa kesho leo kwa kupanda mbegu nzuri na kuzimwagilia kwa imani na upendo kwa watu. Mungu ataleta mvua, jua na ustawi wa mazao yako. Panda mbegu ya msamaha kwa maadui zako, uvumilivu kwa wapinzani wako, tabasamu kwa marafiki zako, mfano bora kwa watoto wako, uchapakazi kwa kazi zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, ndoto kwa malengo yako, na uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli. Kila mbegu irutubishwe kwa mapenzi huru yasiyokuwa na masharti yoyote, au mapenzi huru yasiyokuwa na unafiki wa aina yoyote ile. Usifiche vipaji vyako. Ukiwa kimya utasahaulika. Usipopiga hatua utarudi nyuma. Usiwe na hasira, wivu au ubinafsi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nyota ni kipaji, kipawa, takdiri, karama, au uweza; ni kiashiria cha rohoni kinachoonyesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu, au takdiri ya maisha ya mwanadamu. Unabii na nyota ya ufalme ni kibali cha Mungu katika maisha ya mtu. Kupata kibali hicho, tembea na watu sahihi katika maisha yako (tembea na watu ambao Mungu amekuchagulia kushika funguo za takdiri ya maisha yako). Tamka na kukiri kibali cha Mungu katika maisha yako yote. Panda mbegu za kibali cha Mungu katika udongo wa maisha yako. Jifunze kutenda mema bila malipo, kwani wema ni mbegu ya kibali cha Mungu. Jali mambo ya ufalme wa Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maarifa ni mbegu ya mabadiliko.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mbegu zilizopandwa kwenye udongo wenye rutuba ni rahisi sana kuvamiwa na magugu iwapo mwenye bustani hataipalilia bustani yake kila siku. Kila siku tunapaswa kupalilia bustani zetu za kiroho, kuondoa magugu ambayo ni raha za dunia hii.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mbegu ni neno la Mungu na kudondoka kwake kwenye ardhi si mwisho wa maisha yake. Mambo kadha wa kadha yanaweza kutokea yanayoweza kuathiri ukuaji wa mbegu husika. Nyingine zinaweza kuanguka karibu na njia ndege wakaja wakazila, nyingine zinaweza kuanguka penye miamba pasipokuwa na udongo mwingi wa kutosha, nyingine zinaweza kujifukia ndani kabisa ya ardhi na kupotelea huko kwa miaka mingi, mvua inaweza kunyesha na kuhamisha baadhi ya mbegu kwa kuzisomba na maji. Lakini kwa kuwa maisha yamo ndani ya mbegu, jambo fulani litatokea.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Katika karne iliyopita, wanaakiolojia waligundua mbegu za pamba na ngano katika baadhi ya makaburi waliyokuwa wakiyafukua kwa ajili ya utafiti wao wa kisayansi. Mbegu hizo, zilizokadiriwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 2000 hadi 4000, zilimea na kukua zilipopandwa katika udongo sahihi wenye rutuba. Roho ya maisha ilikuwa bado imo ndani ya mbegu hizo, pamoja na kwamba zilikosa mvua na jua kwa zaidi ya miaka 2000.

Huu ni uthibitisho kwamba kama mbegu itapandwa, itamea na kukua kama itapandwa katika udongo sahihi wenye rutuba. Matumizi sahihi, watu ni ardhi na mazingira yetu na kile tunachokifanya baada ya kupanda mbegu ni neno la ukweli ambalo ndani yake kuna kanuni na mafundisho ya Mungu, ndicho kinachoathiri matumizi ya mbegu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mbegu ni neno la Mungu. Mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni maneno ya Mungu. Kwa hiyo mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni mbegu. Watu ni ardhi. Panda mbegu ya mfano bora kwa watoto wako, msamaha kwa maadui zako, ndoto kwa malengo yako, tabasamu kwa marafiki zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli, uchapakazi kwa kazi zako na uvumilivu kwa wapinzani wako. Kila mbegu irutubishwe kwa imani na upendo kwa watu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mbegu ni neno la Mungu. Mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni maneno ya Mungu. Kwa hiyo mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni mbegu. Watu ni ardhi. Panda mbegu ya mfano bora kwa watoto wako, msamaha kwa maadui zako, ndoto kwa malengo yako, tabasamu kwa marafiki zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli, uchapakazi kwa kazi zako na uvumilivu kwa wapinzani wako. Kila mbegu irutubishwe kwa imani na upendo kwa watu.

Katika mfano huu ukuaji unawakilisha utakaso, ambao ni muundo wa taswira ya Mungu ndani yetu kwa kuishi kama anavyoishi yeye kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Tunachotakiwa kufanya baada ya kupanda mbegu ni kutimiza wokovu wetu sisi wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kutimiza wokovu wetu sisi wenyewe ni sawa na mvua, jua, palizi, mbolea, ili mavuno yaweze kuwa ya uhakika.”
Enock Maregesi