,

Maisha Yako Quotes

Quotes tagged as "maisha-yako" Showing 1-10 of 10
Enock Maregesi
“Katika maisha watu wengi hawataki kukuona ukiendelea kwa sababu ukiendelea unakuwa kioo kwao. Ghafla wataanza kukutazama. Wanajua wana akili kama wewe, wamesoma kama wewe, au wana akili kuliko wewe, au wamesoma kuliko wewe, na labda wanazijua sifa zako za udhaifu na sifa zako za ushupavu toka utotoni kwako. Lakini ghafla unakuwa kioo, na wanapojitazama katika hicho kioo, wanajiona taswira zao isipokuwa sasa hawapo mahali ambapo wewe upo. Katika maisha watu watakushauri, watakufitini, watakurubuni na watakukatisha tamaa. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawaoni unachokiona, hawajui unachokifanya na hawajui unapoelekea. Unachokiona ni takdiri ya maisha yako, unachokifanya ni kupanda mbegu na kuzimwagilia kwa imani, na unapoelekea ni kileleni. Hivyo, songa mbele, kuwa wewe daima, wape muda, wape nafasi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri ('destiny') ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema 'hapana' kwa hiyo 'ndiyo' yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usifanye kazi peke yako wala usiwe mbinafsi! Washirikishe wenzako kukamilisha malengo madhukura ya kadari ya maisha yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usimwabudu mungu mwingine isipokuwa Mungu. Usimwabudu mtu, mnyama, sanamu, samaki, au usiziabudu fikira zako kichwani. Usiitumikie kazi, mali, mila, anasa, siasa, wala usiyatumikie mamlaka au usiutumikie umaarufu au ufahari, kuliko Mungu. Ukiithamini kazi, mali, mila, anasa, siasa au ukiyathamini mamlaka, au ukiuthamini umaarufu au ufahari zaidi kuliko Mungu, au ukiyapa majukumu yako muda mwingi zaidi kuliko Mungu umeabudu miungu; wakati ulipaswa kumwabudu Mungu peke yake. Usiwe na vipaumbele vingine vyovyote vile katika maisha yako zaidi ya Mungu, kwani Mungu ni Mungu mwenye wivu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna siku mbili tu za muhimu zaidi katika maisha yako kama alivyosema Mark Twain: Siku uliyozaliwa na siku uliyojua kwa nini ulizaliwa. Siku utakapojua kwa nini ulizaliwa utakuwa tajiri, wa mali na hekima.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu alikuumba miaka mingi kabla hujazaliwa. Ndani ya roho yako kulikuwa na mpango mkuu wa Mungu juu ya maisha yako katika kipindi chote utakachokuwa hai, na katika kipindi chote utakachokuwa mfu. Lakini Shetani katika mji wa angani unaosemekana kuzuia majibu ya maombi ya Danieli ya siku ishirini na moja, kutoka mbinguni kuja duniani, uitwao Sadiki, wenye mashetani wenye nguvu kuliko mashetani wote katika ufalme wa giza, akaizuia roho hiyo kisha akaiwekea mpango mkuu wa Shetani juu ya maisha yako ili umtumikie yeye badala ya kumtumikia Mwenyezi Mungu.

Kwa mfano, Mungu alipanga uzaliwe mkoani Arusha. Halafu akapanga mke au mume wako azaliwe mkoani Mwanza. Mkoani Arusha Mungu alipanga uwe mwinjilisti wa vitabu, wakati mkoani Mwanza alipanga mke au mume wako awe mwimbaji wa nyimbo za injili. Katika mikoa yote miwili Mungu alishatuma malaika wema wa kuwasaidia katika mipango mikuu ya maisha yenu na kuwaepusha na hila zote za adui.

Lakini badala ya kuzaliwa Arusha au Mwanza Shetani ataziprogramu roho zenu upya ili wa Arusha azaliwe Dodoma au Mara au Venezuela na wa Mwanza azaliwe Lindi au Kagera au Mombasa, ambapo hakutakuwa na malaika wema wa kuwasaidia. Badala ya kuwa mwinjilisti wa vitabu, Shetani atakufanya uwe jambazi; na badala ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za injili, Shetani atakufanya uwe mwanamuziki.

Ndiyo maana wakati mwingine ni vizuri kuhama sehemu unapoishi na kwenda kuishi sehemu nyingine, ambapo kwa kusaidiana na malaika wako wa mwanzo ambaye Mungu alikupangia kabla hujazaliwa, utafanikiwa katika maisha yako, kama alivyofanya Ibrahimu.

Watu wengi wanaishi maisha ambayo si ya kwao. Kukomboa kile ambacho Mungu alikipanga ndani ya roho yako kabla hujazaliwa, na kabla roho yako haijazuiwa na mashetani wa angani, kuwa karibu na Mwenyezi Mungu. Kwa Mungu hakuna siri, atakufunulia tu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Isipite siku hata moja katika maisha yako bila kusema hata kimoyomoyo kwa wazazi wako na kwa watu wote wanaokupenda kwamba unawapenda, kwani siku moja hawatakuwepo tena.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Masharti ya kanuni ya ndoa ya kuachana na ukapera yanakutaka uwe umeshatembea na kukataa asilimia 37 ya wapenzi wako katika kipindi chote cha maisha yako, ili kumpata mpenzi mmoja bora zaidi ambaye ndiye hasa utakayeoa au kuolewa naye.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lakini kanuni hii (‘optimal stopping’) ina walakini. Kwa mfano utajuaje watu au wapenzi utakaotembea nao au kuachana nao katika kipindi chote cha maisha yako? Au itakuaje kama mpenzi wako wa kwanza uliyemwacha ndiye yule ambaye Mungu alikupangia kuwa naye maishani?”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama kuna jambo la muhimu unapaswa kufanya kwa ajili ya kadari ya maisha yako na kipindi hichohicho kuna kipindi kizuri cha televisheni unakisubiria, au simu ya umbea, au kinanda cha shida, palilia bustani yako ya kiroho kwa kuachana na televisheni na simu na kufanya jambo la msingi kwa ajili ya maisha yako.”
Enock Maregesi