,

Maregesi Quotes

Quotes tagged as "maregesi" Showing 1-26 of 26
Enock Maregesi
“Sina jinsi. Nguzo ya maisha yangu ni historia ya maisha yangu. Historia ya maisha yangu ni urithi wa watu waliojifunza kusema hapana kwa ndiyo nyingi – waliojitolea vitu vingi katika maisha yao kunifikisha hapa nilipo leo – walionifundisha falsafa ya kushindwa si hiari. Siri ya mafanikio yangu ni kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu wote; au 'pushing the envelope' kwa lugha ya kigeni.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu hutumia watu 'wajinga' na 'wapumbavu' kufanya mambo makubwa katika maisha yao na ya watu wengine. Katika Biblia, Musa aliitwa mjinga alipokiuka amri ya Farao ya kuendelea kuwafanya watumwa wana wa Israeli nchini Misri; Nuhu aliitwa mpumbavu alipohubiri kwa miaka mia kuhusu gharika, katika kipindi ambacho watu hawakujua mvua ni nini; Daudi aliitwa mjinga alipojitolea kupambana na Goliati bonge la mtu, shujaa wa Gathi; Yusufu aliitwa mjinga alipokataa kulala na mke wa bosi wake, baada ya kuwa ameuzwa na nduguze kama mtumwa nchini Misri; Abrahamu aliitwa mjinga alipoamua kuhama nchi aliyoipenda na kwenda katika nchi ya ahadi, eti kwa sababu Mungu alimwambia kufanya hivyo; Yesu aliitwa mjinga mpaka akasulubiwa aliposema yeye ni Mfalme na Mwana wa Mungu. LAKINI, Musa alitenganisha Bahari ya Shamu na kuwapeleka Waisraeli katika nchi ya ahadi, ambako aliwakomboa kutoka utumwani. Nuhu aliokoa dunia. Daudi alimshinda Goliati. Yusufu aliokoa familia yake kutokana na njaa. Abrahamu alikuwa baba wa imani. Yesu aliyashinda mauti. Wakati mwingine tunatakiwa kufanya mambo makubwa kulingana na jinsi Roho Mtakatifu anavyotutuma, bila kujali watu au dunia itasemaje.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nimewapa watoto wangu kila kitu katika maisha isipokuwa umaskini. Lakini bado wamenishinda.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kolonia Santita ina sura 8 na kila sura ina faslu 3.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Neno moja kutoka mdomoni mwako linaweza kukuletea madhara makubwa. Waweza kusema kitu ukadhani umepatia kumbe umeharibu. Fikiria kwanza maana ya kitu unachosema, halafu sema.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hatutakiwi kuishi kama raia wa Tanzania peke yake. Tunatakiwa kuishi kama raia wa dunia na watumishi wa utu, hasa katika kipindi hiki cha zama za utandawazi. Sina lazima ya kutoka nje kufanya utafiti wa kazi zangu siku hizi. Nje ninayo hapa ndani!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kati ya nchi yako na serikali yako ni kitu gani unakipenda zaidi? Ipende zaidi nchi yako, kuliko serikali yako!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiipenda sana nchi yako ni rahisi sana kuichukia serikali yake!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wape watoto wako urithi wa kutosha ili waweze kufanya kitu, lakini si urithi wa kutosha ili wasiweze kufanya kitu. Wape watoto uhuru wanaostahili kupata, uhuru wa mahesabu, lakini si uhuru wa kila kitu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiwapa watoto wako uhuru wa shaghalabaghala au uhuru wa kila kitu watajisahau! Wape uhuru wa mahesabu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maana halisi ya falsafa ya 'Nitakuwa tayari kufungwa kwa ajili ya matatizo ya watu', au Falsafa ya Kufungwa, ni uvutano mkubwa uliopo kati ya Roho Mtakatifu na Roho wa Shetani kwa sisi wanadamu wote. Jambo lolote baya limtokealo mwanadamu husababishwa na Shetani na si Mungu na watu hupata matatizo kwa sababu ya kudharau miito ya mioyo yao wenyewe, au kudharau kile Roho Mtakatifu anachowambia. Unaweza kuvunja sheria kwa manufaa ya wengi kwani mibaraka haikosi maadui. Ukifungwa kwa kuvunja sheria kwa ajili ya manufaa ya wengi watu watakulaani lakini Mungu atakubariki. Kwa nguvu ya uwezo wa Roho Mtakatifu Mungu atamshinda Shetani kwa niaba yako. Tukijifunza namna ya kuwasiliana na Roho Mtakatifu hatutapata matatizo kwani Mungu anataka tuishi kwa amani katika siku zote alizotupangia, licha ya damu yetu kuwa chafu. Mtu anapokufa kwa mfano, Roho wa Shetani amemshinda Roho Mtakatifu na Roho Mtakatifu hatalipendi hilo kwa niaba ya Mungu. Ikitokea mtu akayashinda majaribu ya Shetani katika kipindi ambacho watu wote wameyashindwa; mtu huyo amebarikiwa na Mungu, ili aitumie mibaraka hiyo kuwaepusha wenzake na roho mbaya wa Shetani.
Nikisema 'Kwa nguvu ya uwezo wa Roho Mtakatifu Mungu atamshinda Shetani kwa niaba yako' namaanisha, Roho Mtakatifu ana uwezo wake na Roho wa Shetani ana uwezo wake pia. Ukimshinda Roho wa Shetani uwezo wa Roho Mtakatifu umekuwa mkubwa kuliko uwezo wa Roho wa Shetani, na ukishindwa kumtii Roho Mtakatifu uwezo wa Roho wa Shetani umekuwa mkubwa kuliko uwezo wa Roho Mtakatifu, ilhali uwezo wa Mungu ni mkubwa kuliko wa Roho Mtakatifu na wa Roho wa Shetani kwa pamoja. Mungu humtumia Roho Mtakatifu kumlindia watoto wake ambao ni sisi dhidi ya Shetani … Kila akifanyacho Roho Mtakatifu hapa duniani ni kwa niaba ya Mungu, na tukimtii Roho Mtakatifu Mungu atamshinda Shetani kwa niaba yetu. Mtu anapofungwa kwa kutetea maslahi ya umma wewe unayemfunga umemtii Roho wa Shetani. Yule anayefungwa amemtii Roho Mtakatifu maana amebarikiwa, na mibaraka haikosi maadui.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuwa mwangalifu unapoongea na watu. Huwajui!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Sikujui. Lakini naamini hungependa kuishi maisha yako hapa duniani bila kuacha urithi au kumbukumbu ya aina yoyote katika jamii. Zifuatazo ni ngazi tano muhimu zitakazofanya uache dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta: Tambua vitu vya muhimu katika maisha yako ijapokuwa unaweza kuacha alama katika dunia bila kujitambua baada ya kuondoka; Tumia kipaji ulichopewa na Mungu; Fanya kazi kwa bidii na maarifa; Shindana na wenzako kuwa juu zaidi katika tasnia uliyojichagulia; Kuwa makini na kila kitu unachofanya kwa maana ubongo ni kitu cha ajabu, ubongo una uwezo wa kukupotosha.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukitambua vitu vya muhimu katika maisha yako hapa duniani na kuvipa kipaumbele cha kwanza, ukatumia kipaji ulichopewa na Mungu na ukafanya kazi kwa bidii na maarifa, halafu ukashindana na wenzako kuwa juu zaidi katika tasnia uliyojichagulia, ukafanya kila kitu kwa makini ukihofia maamuzi ya ubongo wako, utaacha urithi kwa faida ya vizazi vijavyo. Kuwa na akili, kuwa na uwezo wa kujiwekea malengo, kuwa mchapakazi hodari. Namna hiyo, hakuna kitakachoweza kushindikana.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Sikujui. Lakini naamini hungependa kuishi maisha yako hapa duniani bila kuacha urithi au kumbukumbu ya aina yoyote katika jamii.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tambua vitu vya muhimu katika maisha yako ijapokuwa unaweza kuacha alama katika dunia bila kujitambua baada ya kuondoka.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuwa makini na kila kitu unachofanya kwa maana ubongo ni kitu cha ajabu, ubongo una uwezo wa kukupotosha.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Heri kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka, kuliko kusema mbele za watu kwamba pesa haijakupa furaha. Wengi hupata jeuri ya kusema hivyo kutokana na umaskini wa watu wanaowazunguka.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini mwenye pesa nyingi ni tajiri bahili. Tajiri mwenye mifuko iliyotoboka ni tajiri badhiri.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukitaka kufanikiwa katika maisha yako kuwa tayari kuitwa mjinga au mpumbavu.”