Willy Puchner
Willy Puchner ni mtu kutoka nchi ya Austria, amezaliwa tarehe 15 Machi 1952. Puchner ni mpiga picha, msanii, mchoraji na mtunzi.
Historia yake
[hariri | hariri chanzo]Puchner amezaliwa na kulelewa kijijini Mistelbach an der Zaya, Austria ya Chini, ambako wazazi wake walikuwa na studio ya kupigia picha. Mnamo mwaka 1967 alihamia Vienna alikokwenda kujifunza upigaji wa picha katika Taasisi ya Utafiti na Mafunzo ya Shirikisho la Vienna iliyo chuo cha sanaa ya picha. Baada ya kuhitimu mwaka 1974, alifanya kazi ya ukufunzi katika chuo hicho kwa miaka miwili. Kuanzia mwaka 1978, Puchner alifanya kazi kama mpiga picha na mwandishi wa kujitegemea akiwa na makazi yake jijini Vienna hadi mwaka 1983 alipoanza mafunzo ya falsafa, historia na elimu ya jamii.
Puchner alihitimu mafunzo hayo na kupata Shahada ya Uzamili katika somo la falsafa mnamo mwaka 1988. Tasnifu yake aliiita "Über private Fotografie" (Kijerumani kwa "Upigaji picha wa watu binafsi"). Kuanzia mwaka 1988 ametoa mihadhara mbali mbali juu ya "Upigaji picha wa watu binafsi" katika vyuo vikuu, nyumba za makumbusho na vituo vya maonyesho. Kuanzia mwaka 1989 Puchner amekuwa akifanya kazi mara kwa mara na hufanya kazi na gazeti la "Wiener Zeitung", (gazeti la zamani la kila siku kuliko gazeti lolote duniani).
Vile vile, Willy Puchner hupendelea kufanya kazi na watu wenye umri mkubwa na alianzisha miradi kama "Die 90 jährigen" (Wenye umri wa miaka 90), "Dialog mit dem Alter" (Mjadala na uzee), "Die 100-jährigen" (Wenye umri wa miaka 100), "Lebensgeschichte und Fotografie" (Wasifu na upigaji picha) na "Liebe im Alter" (Mapenzi katika uzee).
Maonyesho
[hariri | hariri chanzo]- Museum Moderner Kunst (Museum of Modern Art), Vienna (Austria)
- Künstlerhaus (House of Artists), N.Ö. Galerie, Vienna (Austria)
- Museum des 20. Jahrhundert (Museum of the 20th Century), Vienna (Austria)
- Steirischer Herbst, Graz
- Berlin, Bremen, Kleve, Braunschweig (Ujerumani)
- Norfolk, Washington, (Marekani)
- Bombay (India)
- Beirut (Lebanon)
- Tokyo, Osaka, Oita, Nagoya, Sapporo (Ujapani)
Machapisho
[hariri | hariri chanzo]Extrablatt, konkret, Stern, Geo, Life, Mare, Corriere della Sera, Marco Polo, Universum, Falter, Wiener Zeitung
Maandiko ya historia ya maisha
[hariri | hariri chanzo]- Bäume, 1980, (Text Henry David Thoreau), ISBN 3-85447-271-4
- Zum Abschied, zur Wiederkehr, 1981 (Text Hermann Hesse), ISBN 3-20601-222-8
- Gestaltung mit Licht, Form und Farbe, 1981, ISBN 3-87467-207-7
- Strahlender Untergang, (Text Christoph Ransmayr), 1982, ISBN 3-85447-006-1
- Andalusien, 1983, ISBN 3-7658-0420-7
- Die Wolken der Wüste, 1983 (mit einem Text von Manfred Pichler), ISBN 3-89416-150-7
- Dorf-Bilder, 1983, ISBN 3-21800-387-3
- Zugvögel seit jeher, 1983, (Text Erich Hackl), ISBN 3-21024-848-6
- Das Herz des Himmels, 1985, (Text Erich Hackl), ISBN 3-21024-813-3
- Die Sehnsucht der Pinguine, 1992, ISBN 3-44617-200-9
- Ich bin ..., 1997, ISBN 3-79182-910-6
- Tagebuch der Natur, 2001, ISBN 3-85326-244-9
- Flughafen. Eine eigene Welt, 2003, ISBN 3-85326-277-5
- Illustriertes Fernweh. Vom Reisen und nach Hause kommen, 2006,.ISBN 3-89405-389-5
- Wien. Vergnügen und Melancholie, 2008, ISBN 3-85033-159-8