Nenda kwa yaliyomo

Tomaso wa Villanova

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Mt. Tomas (Madrid, 1791).

Tomaso wa Villanova, O.S.A. (awali Tomás García y Martínez; Villanueva de los Infantes, 1488Valencia, 8 Septemba 1555) alikuwa mtawa Mwaugustino kutoka Hispania maarufu kama mhubiri na mwandishi.

Hatimaye alikubali kwa utiifu tu kuwa askofu mkuu; hapo, pamoja na maadili mengine ya mchungaji bora, aliwaka upendo mkubwa sana kwa maskini wa jimbo lake akawashughulikia hata kumaliza mali yake yote, asibaki hata na kitanda kidogo cha kukilalia [1].

Papa Aleksanda VII alimtangaza mtakatifu tarehe 1 Novemba 1658.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: