Tashtiti
Tashtiti (kwa Kiing. rhetorical question) ni mbinu ya kuuliza swali kwa jambo ambalo unafahamu jibu lake, na hufanya hivyo kwa lengo la kusisitiza jambo, kuleta mshangao, n.k.
- Mfano
- Ikiwa mtu kapoteana na rafiki yake kwa muda mrefu, halafu ghafla wanakutana, huweza kumwuliza "Aisee! ni wewe?", hali anajua kuwa ni yeye.
Tashtiti katika fasihi
Katika fasihi tashtiti (kiing. satire) ni mbinu inayolenga kukosoa maovu, ujinga, unyanyasaji na kasoro kwa namna ya kejeli au utani, mara nyingi kwa shabaha ya kuhamasisha maboresho.
Mara nyingi aina mbili za tashtiti hutofautishwa zinazolinganishwa na mbinu tofauti za wanatashtiti Horatius na Juvenal wa Roma ya Kale.
Tashtiti ni mbinu ambayo imetumiwa na watunzi kutaja yasiyotajika bila kuchukiza, kuchukuliwa vibaya au kumuudhi msomaji. Tashtiti huwasilisha maudhui nyeti kwa njia ya ucheshi. Tashtiti haiibui tu ucheshi bali ni ucheshi wenye lengo la kurekebisha.[1]
Tanbihi
- ↑ Ayodi, Beja, Ogola: Tashtiti na Wanatashtiti, maana, umuhimu na vipengele vyake katika fasiki; Mulika na. 33, uk. 46-57
Marejeo
- Nyambari Nyangwine, J.A Masebo - Jitayarishe kwa Kishwahili Toleo Jipya, 2008. ISBN 978 9987 09 017 4.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |