Nenda kwa yaliyomo

Sophokles

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nususanamu ya Sophocles

Sofokles (pia: Sophokles; Kigiriki Σοφοκλῆς alizaliwa mnamo 496 KK, alikufa 406 KK) alikuwa mshairi na mwandishi wa Ugiriki ya Kale anayekumbukwa pamoja na Aeschylos and Euripides kama mmoja wa watungaji wakuu watatu wa michezo tanzia wa ustaarabu huu wa Kigiriki. Alitunga michezo zaidi ya 120 na 7 imehifadhiwa hadi leo mengine inajulikana kwa jina au kisehemu tu.

Alikuwa raia wa mji wa Athens na kwa muda wa miaka 50 alikuwa mwandishi aliyeshinda mashindano ya shairi na tamthiliya mengi yaliyofanywa kila mwaka.

Sofokles aliendeleza mchezo tania uliokuwa hadi yake na waigizaji wawili tu pamoja na kwaya kwa kumwongeza mwigizaji wa tatu. Kwa nia hiyo aliwapa waigizaji nafasi kushinda kwaya.

Pamoja na uandishi michezo na maigizo alishiriki pia katika maisha ya kisiasa ya mji wake. Katika muundow a demokrasia ya Athens alishiriki katika vyeo vya muda kama kuchaguliwa kuwa kiongozi wa jeshi, kuhani wa hekalu, mtunza hazina wa dola na mengine.

Maigizo yake

[hariri | hariri chanzo]

Kati ya maigizo yaliyohifadhiwa ni

  • Antigone
  • Oedipus Mfalme
  • Oedipus mjini Kolonos
  • Ajax
  • Elektra
  • Philoktetes
Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Ulaya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sophokles kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.