Nenda kwa yaliyomo

Q

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz

Q ni herufi ya 17 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia alfabeti ya Kiswahili. Haitumiki katika mwandishi wa maneno ya Kiswahili isipokuwa kwa maneno ya kigeni.

Hapo sauti yake huwa ni "k". Hutokea mara nyingi pamoja na "u" kama "Qu" kwa sauti za "ku", "kw" au "kv". Hutumiwa pia kwa sauti ya ق (qaf) au "k ya shingoni" katika maneno ya Kiarabu kama vile "Qatar" yakiandikwa kwa alfabeti ya Kilatini.


Historia

[hariri | hariri chanzo]
Kifinisia Qof Kigiriki Koppa Kietruski Q Kilatini Q
Lateinisches Q

Asili ya Q ni alama ya Qof katika mwandiko wa Kifinisia. Hakuna uhakika kuhusu maana asilia ya alama hiyo lakini herufi zote za Kifinisia zilitokana na picha zilizorahisishwa. Ilitumiwa kwa sauti ya "k ya shingoni" jinsi ilivyo hadi leo katika qaf ya Kiarabu.

Wagiriki wa Kale walipokea herufi za Wafinisia na kuziendeleza. Hawakuwa na sauti kama ile "qof" ya kifinisia. Awali waliita herufi hii "koppa" na kuitumia kwa sauti ya "k" kabla ya "o" na "u" lakini baadaye hawakuona faida tena ya kuwa na alama mbili kwa "k" ileile wakafuta koppa.

Alfabeti ya Kigiriki ilitumiwa na Waetruski huko Italia wakati "koppa" bado ilikuwemo. Waliendelea kuitumia kwa sauti ya "ku" iliyotokea mara nyingi katikla lugha yao. Waroma wa Kale walipokea hivyo kutoka kwa Waetruski katika Kilatini. Mstari wa chini ukasogea kando jinsi ilivyo hadi leo.