Mwani
Mwani | ||
---|---|---|
Saladi ya bahari (Ulva lactuca)
| ||
Uainishaji wa kisayansi | ||
| ||
Ngazi za chini | ||
Makundi bila nasaba:
|
Miani (kwa Kiing. algae) ni kundi kubwa la viumbehai vinavyofanana na mimea. Spishi ndogo huitwa viani au vijimea. Zina uwezo wa kujilisha kwa njia ya usanisinuru yaani hutengeneza chakula chao kwa msaada wa mwanga wa jua. "Viani kijanibuluu" siyo viani vya kweli lakini kundi la bakteria: Sianobakteria.
Kundi hili si kundi rasmi la kibiolojia au taksoni, kwa sababu vikundi vya miani havina na uhusiano mara kwa mara au ni polifiletiki (Kiing. polyphyletic).
Kuna aina nyingi sana za miani. Nyingine zina seli moja tu na nyingine zina seli nyingi. Spishi kubwa zinajulikana sana na huitwa miani tu au mwani wa bahari. Katika uwezo wa usaninisinuru zinalingana na mimea lakini hukosa viungo vingi vilivyo kawaida kati ya mimea hivyo katika taksonomia au mpangilio wa spishi hazihesabiwi kati ya mimea.
Miwani haina majani, mizizi wala viungo vyingine vya mimea.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Dinobryon ni mwani wa ngeli ya Chrysophyceae
-
Mwani wa Laurencia katika hadubini: matawi yake ni mfuatano wa seli za pekee na yote ina unene wa mm 1 pekee
-
Viani aina ya fitoplanktoni vikiota kama maua katika Atlantiki ya Kusini mbele ya Argentina