Melvin Schwartz
Melvin Schwartz (2 Novemba 1932 - 28 Agosti 2006) alikuwa mwanafizikia Mmarekani. Mwaka 1988 alipokea Tuzo ya Nobel ya Fizikia pamoja na Leon Max Lederman na Jack Steinberger kwa mafanikio yao ya kugundua mbinu za kushughulika maneutrino ambazo ni chembe ndogo sana ya kinyuklia isiyo na chaji na haipasuliki.
Alikuwa mtoto wa mji wa New York akasoma Bronx High School of Science na chuo kikuu cha Columbia University alipokuwa mwanafunzi wa mshindi wa Tuzo Nobel Isidor I. Rabi na profesa msaidizi tangu 1958.
Mwaka 1966 alihamia Chuo Kikuu cha Stanford alipokuta mashine mpya ya kuharakisha mwendo wa chembe za kinyuklia iliyomsaidia kuendeleza utafiti wake.
Mwaka 1991 akawa mkurugenzi msaidizi wa idara ya fizikia ya kinyuklia kwenye taasisi ya Brookhaven National Laboratory (yaani Maabara ya Kitaifa kule Brookhaven, Marekani) alipowahi kutekeleza majaribio yake yaliyompatia tuzo ya Nobel baadaye. Wakati ule akawa pia profesa kamili huko Columbia.
Alistaafu mwaka 2000.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Melvin Schwartz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |