Nenda kwa yaliyomo

Max Weber

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Max Weber mnamo 1894.

Maximilian Carl Emil Weber (21 Aprili 186414 Juni 1920) alikuwa mwanasheria na mtaalamu wa siasa na sayansi ya jamii nchini Ujerumani.

Alisoma sheria, uchumi, falsafa na historia kwenye vyuo vikuu vya Heidelberg, Berlin na Göttingen.

Mwaka 1889 alichukua cheo cha dokta wa sheria kwenye chuo kikuu cha Berlin.

Akaendelea kuwa profesa wa uchumi huko Freiburg na tangu mwaka 1897 kwenye chuo kikuu cha Heidelberg.

Mwaka 1889 aliondoka kwenye chuo kikuu kutokana na ugonjwa, akaendelea kuhariri gazeti la sosholojia na kuandika vitabu.

Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia alikuwa mshauri wa serikali ya Ujerumani kwenye majadiliano kwa ajili ya mkataba wa Versailles na ndani ya Ujerumani alikuwa kati ya waanzilishi wa chama huria cha demokrasia.

Mwaka 1919 alianza kufundisha tena kwenye chuo kikuu lakini mwaka 1920 alifariki dunia.

Maandishi

[hariri | hariri chanzo]

Weber aliandika mengi kuhusu uchumi, utawala, siasa na dini.

Kati ya maandiko yaliyokuwa mashuhuri hasa ni "Maadili ya Kiprotestanti na roho ya ubepari" (Die protestantische Ethik und der 'Geist' des Kapitalismus). Humo alitoa hoja ya kuwa Uprotestanti, hasa kadiri ya Yohane Kalvini, ulisababisha wafuasi wake kubana matumizi ya fedha kwa maisha tajiri na kuridhika maisha ya wastani hata kama wamefaulu kiuchumi. Maadili hayo yaliwawezesha kukusanya rasilimali iliyokuwa msingi muhimu kwa mapinduzi ya viwandani.

Pia imani ya kutisha katika uteule, iliyodai utajiri ni baraka ya Mungu unaoashiria kuwa mhusika ataokoka milele, iliwafanya waamini hao wajitahidi kupata mali ili wajisikie salama mbele ya hukumu ya mwisho.

Kwake ndiyo mambo yaliyochangia kuhamishia Kaskazini mwa Ulaya (ulikoenea Uprotestanti) usukani wa uchumi kutoka nchi za Kusini zilizobaki katika Kanisa Katoliki.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

Maandishi ya Weber

[hariri | hariri chanzo]

Kuhusu Weber

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Max Weber kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.