Nenda kwa yaliyomo

Kufa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Kufa nchini Irak
Al Kufa G.Msikiti katika Jiji la Kufa huko Najaf nchini Iraq
Al Kufa G.Msikiti katika Jiji la Kufa huko Najaf nchini Iraq

Kufa (pia: Kofa; kwa Kiarabu الكوفة, al-kūfah) ni mji wa Irak wenye wakazi 110,000 .

Uko takriban 170 km kusini kwa Baghdad na 10 km kaskazini kwa Najaf kando ya mto Frati.

Kama mahali pa mauti ya Imam Ali, Kufa pamoja na Samarra, Karbala na Najaf ni kati ya miji minne mitakatifu ya Washia nchini Irak.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mji ulijulikana kwa jina la Surestan katika milki ya Uajemi wa Kale.

Baada ya uvamizi wa Kiislamu mwaka 637 palikuwa na kambi kubwa la kijeshi lililoendelea kuwa mji mkuu wa kwanza wa Uislamu. Wanajeshi Waislamu 30,000 walipelekwa hapo kama walowezi. Khalifa Ali ibn Abu Talib alipeleka makao makuu yake hapo mwaka 656 akafa mjini mwaka .

Mwaka 749 Waabbasi baada ya kupindua Wamuawiya walifanya Kufa mji mkuu wa khilafa hadi 762 walipohamia Baghdad.

Kurani kwa mwandiko wa Kikufa, karne ya 8

Umuhimu wa Kufa ulipungua kisiasa lakini uliendelea kiutamaduni hadi karne ya 11. Mji ulikuwa kitovu cha teolojia ya Kiislamu na masomo ya Kurani. Abu Hanifa, mwanzilishi wa mkondo wa maelezo ya fiq, alikuwa mtu wa Kufa. Mtindo wa kwanza wa mwandiko wa Kiarabu huitwa "Mwandiko wa Kufa" hadi leo.

Baada ya karne ya 11 mji uliharibiwa vitani mara kwa mara ukaanza kupungua sana hadi kukua tena katika karne ya 20.