Kizuizi cha hamu ya chakula
Kizuizi cha hamu ya chakula (kwa Kiingereza: anorectic au anorexic) ni aina ya dawa ambayo mtu hupewa ili kupunguza uchu wa chakula na kwa njia hiyo kumwezesha kupunguza uzani.
Kwa watu wanaotaka kupunguza uzani mwilini (weight losers), kuzuia hamu ya chakula ni jambo muhimu. Unapozuia hamu ya chakula, utapata kula kidogo bila ule uchu wa kutaka chakula kingi hata wakati huna njaa.
Jamii nyingi za Afrika, hasa kule Kusini kunako jangwa la Kalahari, wamebobea katika kula matunda aina ya Hoodia Gordooni ambayo huwafanya wahisi kana kwamba hawana njaa, hivyo kuweza kuendelea kwa muda mrefu katika malisho yao bila ule uchu wa kutaka kula.
Tunda linalofanana na mboga la "garcinia cambogia" limekuwa likitumika pia kwa muda mrefu kwa kuzuia hamu ya chakula.
Vizuizi hivi hufanya ubongo wa mwanadamu uhisi kana kwamba hana njaa hata wakati tumbo lake linaponguruma.
Wanaotaka kupunguza uzani hufurahishwa na jambo hili kwa maana wanaweza kula chakula kidogo bila hamu ya kuzidisha. Vizuizi hivi pia huwafanya wasiage chakula kidogo walichokula na kutoa nguvu mwilini za mazoezi.
Baadhi ya madawa haya ya kuzuia hamu ya chakula ni pamoja na "Unique hoodia" kutokana na mmea wa Hoodia goodoni, "Garcinia extra" kutokana na mboga ya Garcinia cambogia. Mengine ni phenq na phen375 kutokana na phentamine.
Kabla ya kumeza tembe hizi za kuzuia hamu ya chakula, wagonjwa kwanza hupewa dawa au kinywaji cha kusafisha tumbo. Dawa hii huufanya utumbo uondoe ufuta na vitu vingine vilivyokuwa vikifanya mwili wa mtu uitishe chakula kingi. Baada ya kusafisha mwili, mtu huweza kudhibiti chakula anachokila.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kizuizi cha hamu ya chakula kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |