Nenda kwa yaliyomo

Jeradi Edwards

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wafiadini wa Oaten Hill (Robert Wilcox, Gerard Edwardes, Christopher Buxton na Robert Widmerpool).

Jeradi Edwards (pia alijiita: Edward Campion; Ludlow, Shropshire, 1552Canterbury, 1 Oktoba 1588) alikuwa padri kutoka Uingereza.

Baada ya kupewa upadrisho huko Ufaransa (1587), alirudi nchini ili kufanya utume kwa siri ila alikamatwa na, baada ya kufungwa gerezani muda mrefu, hatimaye alinyongwa pamoja na mapadri wenzake Robati Wilcox na Kristofa Buxton na mlei Robati Widmerpool aliyesaidia utume kama huo wakati wa dhuluma ya malkia Elisabeti I[1].

Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929 na mtakatifu na Papa Paulo VI mwaka 1976.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 1 Oktoba[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.