Nenda kwa yaliyomo

Daraja la Umoja 2

Majiranukta: 11°34′46″S 35°25′46″E / 11.5795°S 35.4295°E / -11.5795; 35.4295
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

11°34′46″S 35°25′46″E / 11.5795°S 35.4295°E / -11.5795; 35.4295 Daraja la Umoja 2 (kwa Kiingereza Unity Bridge 2) ni daraja linalovuka mto Ruvuma na kuunganisha Wilaya ya Songea Vijijini na Mkoa wa Niassa, Msumbiji. Liko upande wa kusini wa Mji wa Songea karibu na sehemu ambako Ruvuma inabadilisha mwelekeo wake kwenda mashariki na kuwa mpaka baina ya Tanzania na Msumbiji.

Daraja linafikiwa kwa kilomita 180 za barabara ya vumbi kutoka Songea mjini. Ni tofauti na daraja lingine la mto Ruvuma linaloitwa "Daraja la Umoja 1" lililopo takriban kilomita 330 upande wa magharibi katika Mkoa wa Mtwara.

Upande wa Tanzania mpaka unaitwa Mkwenda. Upande wa Msumbiji miji ya karibu ni Matchedje na Lipulichi.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Daraja la Umoja 2 kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.