Po (mto)
Po ni mto mrefu zaidi nchini Italia, wenye urefu wa kilomita 652.
Mto Po | |
---|---|
| |
Chanzo | Milima ya Monviso |
Mdomo | Bahari ya Adria |
Nchi za beseni ya mto | Italia (100.0%) |
Urefu | 652 km |
Unapita kaskazini mwa Italia kuanzia chanzo chake katika milima ya Alpi kuelekea mashariki hadi mdomo wake kwenye bahari ya Adria karibu na mji wa Venisi.
Beseni lake huwa na eneo la km² 71,000.
Unapitia mikoa minne: Piemonte, Lombardia, Emilia-Romagna, Veneto. Hapo unapita kwenye miji muhimu kama vile Torino na karibu na Milano.
Mdomo wake huishia kama delta.
Picha
hariri-
Mto Po mwanzoni mwa mwendo wake
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Po (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |