Sagita (kundinyota)
Sagita (kwa Kilatini na Kiingereza Sagitta) [1] ni jina la kundinyota ndogo iliyopo kwenye nusutufe ya kaskazini ya Dunia.
Mahali pake
[hariri | hariri chanzo]Sagita (Sagitta) lipo karibu na nyota angavu za Vega na Tairi. Inapakana na makundinyota jirani ya Mbweha (Vulpecula), Rakisi (Hercules), Ukabu (Aquila) na Dalufnin (Delphinus)'.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Sagita (Sagitta) lilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema السهم as-sahm kwa maana ya “mshale” [2]. Waarabu walitafsiri hapa jina la Ptolemaio aliyetaja nyota hizi vile kwa jina la Βέλος Velos katika orodha yake ya Almagesti.
Sagitta - Sagita ni kati ya makundinyota 48 yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika kitabu cha Almagesti wakati wa karne ya 2 BK. Lipo pia katika orodha ya makundinyota 88 yaliyorodheshwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [3] kwa jina la Sagitta. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni 'Sge'.[4]
Nyota
[hariri | hariri chanzo]Nyota angavu zaidi ni Gamma Sagittae. Ina mwangaza unaoonekana wa mag 3.5 ikiwa na umbali wake unakadiriwa kati ya miakanuru 258 kutoka Dunia[5][6].
Jina la (Bayer) |
Namba ya Flamsteed |
Jina (Ukia) |
Mwangaza unaoonekana |
Umbali (miakanuru) |
Aina ya spektra | |||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
γ | 12 | 3,5m | M0 III | |||||||
δ | 7 | 3,7m | M2 II + B6 | |||||||
β | 6 | 4,4m | G8 IIIa | |||||||
α | 5 | Sham | 4,4m | - |
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Uhusika milikishi (en:genitive) ya "Sagitta" katika lugha ya Kilatini ni "Sagittae" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Sagittae, nk.
- ↑ ling. Knappert 1993; anarejelea jina la Kiarabu kuwa "Sahm al Hamsa" yaani "mishale mitano"
- ↑ The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
- ↑ Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy. 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R.
- ↑ Sagitta, tovuti ya Constellation Guide, iliangaliwa Oktoba 2017
- ↑ Gammaa Sagittae, tovuti ya Prof. Jim Kaler
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Constellation Guide: Sagitta constellation
- Sagitta, "Stars", kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
- Star Tales – Sagitta, tovuti ya Ian Ridpath, iliangaliwa Oktoba 2017
- The Deep Photographic Guide to the Constellations: Sagitta
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Argo Navis” ukurasa 131 ff (online hapa kwenye archive.org)
- Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331