Mwamba mashapo
Miamba mashapo (kwa Kiingereza: sedimentary rocks) hutokea pale ambapo mashapo hukaa kwa muda mrefu yakifunikwa na mashapo mengine na kuathiriwa na uzito wa matabaka ya juu yanayosababisha shinikizo kubwa. Miamba ya aina hiyo hufanya sehemu kubwa ya uso wa ardhi, ingawa Dunia kwa jumla kuna zaidi miamba ya mgando (igneous rocks) na miamba metamofia (metamorphic rocks).
Asili ya miamba mashapo
[hariri | hariri chanzo]Mashapo kwa kawaida ni mata inayokusanyika chini kwenye mito, maziwa na bahari baada ya kupelekwa huko na mwendo wa maji, kiasi pia kwa mwendo wa upepo. Mata ya mashapo ni pamoja na vipande vidogo vya mawe yaliyosagwa au kuvunjikavuunjika, mabaki ya mimea au wanyama na mata yaliyotokana na utendanaji wa kikemia.
Aina za miamba mashapo
[hariri | hariri chanzo]Miamba mashapo inapatikana hasa ya aina tatu: gange (mawe ya chokaa, limestone), jiwe mchanga (sandstone) na mwambatope (shale). [1]
Miamba mashapo hufunika asilimia 75 – 80 za uso wa ardhi, lakini hufanya 5% tu za ganda la Dunia. Viwango husianifu wa aina za miamba mashapo ni kama ifuatavyo:
- Mwambatope ---------- 60%
- Jiwe la mchanga-- 20%
- Gange (CaCO3) --- 15%
- Mengine ----- 5%
Kuimarishwa
[hariri | hariri chanzo]Kama mashapo yameshinikizwa kwa nguvu ya kutosha kwa muda mrefu, huimarishwa na kugeuka kuwa mwamba thabiti. Iliyopandwa na kushinikizwa kwa muda, matope huwa 'yameunganishwa' (yamefanywa kuwa thabiti) kuwa safu ya mwamba. Katika mwamba huo matabaka yanatambulika yanayoonyesha jinsi gani mashapo yalivyojipanga wakati wa kushuka kwenye tako la bahari na kufunikwa na matabaka mapya.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Blatt H; Middleton G. & Murray R. 1980. Origin of sedimentary rocks. Prentice-Hall.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]The Wikibook Historical Geology has a page on the topic of |
- Basic Sedimentary Rock Classification Archived 23 Julai 2011 at the Wayback Machine., by Lynn S. Fichter, James Madison University, Harrisonburg.VI;
- Sedimentary Rocks Tour, introduction to sedimentary rocks Archived 7 Septemba 2016 at the Wayback Machine., by Bruce Perry, Department of Geological Sciences, California State University at Long Beach .
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwamba mashapo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |