Walarasi
Nguva aktiki | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Nususpishi 3:
|
Nguva aktiki (Odobenus rosmarus, pia huitwa: Walrosi kutoka Kiing. Walrus) ni mnyama mkubwa wa Bahari ya Aktiki anayefanana na nguva wa kahawia mwenye meno mawili marefu, pia yaitwa pembe, kama tembo.
Etimolojia
Jina la nguva aktiki linatoka neno la nguva kwa sababu mara nyingi mnyama huyu mara amechanganyikiwa na nguva halisi. Lakini neno la walrosi linatoka neno la Kiingereza walrus litokalo neno la Kiholanzi walvis (nyangumi) na ros (farasi).
Anatomia
Vifuko vya hewa chini ya koo shingoni mwa nguva aktiki, shingo lililo fupi na nene, vifuko hivyo vina uwezo wa kuvimba na hewa ili kumpa uwezo wa kuelea wima na kichwa chake juu ya maji. Pia vinatumiwa kama vyumba vya mvumo vinavyotoa sauti kama kengele chini ya maji. Kinyume ya vikono vya nyuma, haya ni marefu kama yaliyo mapana, lakini yana unene na gegedu na vidole vitano kama vikono vya nyuma. Wanapoogelea, yanatumiwa mara kwa mara kupiga kasia katika mwendo ulio chini lakini mara nyingine hutumiwa kuelekeza. Masikio yao madogo yana kunyanzi ya ngozi nje yao ili kufanya vichwa vyao vinyooke ili waogelee vyema zaidi majini. Nguva aktiki ni mdogo kuliko tembo-bahari aliye mkubwa kabisa kati ya Pinnipedia (wanyama wenye miguu-mapezi).
Pembe
Zimeundwa na dentini, pembe za nguva aktiki ni ndefu sana na ni meno yanayoendelea kukua. Hazitumiwi kuchimbia chakula lakini huwapea usaidizi mwingi wanapojikokota barafuni au ardhini. Pia zinatumiwa kuonyesha utawala na cheo.
Ngozi
Ngozi ni ya hudhurungi yenye kunyanzi inayoonekana kama inabadilisha rangi kulingana na halijoto, kwa sababu wakati anapohisi joto, utiririshi wa damu kuelekea usoni mwa ngozi huongezeka ili kumpoza. Tendo hili humpatia nguva aktiki sura nyekundunyekundu na huonekana kama ana madoadoa. Anapohisi baridi, utiririshi wa damu kuelekea usoni mwa ngozi hupunguzika, kumpatia sura ya kukwajuka. Tabaka ya shahamu kubwa iliyo na upana wa hadi sentimita 15 inayomkinga kutoka kwa baridi.
Sharubu
Sharubu zao zilizo puani ni nene na zina hali ya juu ya kuhisi na husaidia wanapotafuta chakula.