Liturujia ya Trento
Liturujia ya Trento ni taratibu za ibada zinavyotumiwa na baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki kufuatana na mapokeo ya Roma jinsi yalivyokuwa mwaka 1962.
Mabadiliko ya liturujia yaliyofanywa baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano (1962-1965), baadhi yakiwa halali na baadhi kinyume cha sheria za Kanisa, yalisababisha upinzani mkali kutoka kwa wapenzi wa taratibu za awali, ambazo kwa kiasi kikubwa zilipangwa na Papa Pius V baada ya Mtaguso wa Trento na kwa sababu hiyo pengine zinaitwa liturujia ya Trento.
Mwaka 2007 Papa Benedikto XVI kwa hati Summorum Pontificum [1] alipanua ruhusa ya kutumia taratibu hizo duniani kote kama namna isiyo ya kawaida ya liturujia ya Roma.[2]
Tathmini iliyofanywa mwaka 2020 ilionyesha ruhusa hiyo haikutumika vizuri, hivyo Papa Fransisko kwa hati Traditionis Custodes ya tarehe 16 Julai aliifuta kwa jumla akimwachia askofu wa jimbo uamuzi kuhusu maombi ya kutumia taratibu hizo, mradi isiwe parokiani.
Tanbihi
hariri- ↑ Summorum Pontificum in Latin and English Archived 10 Oktoba 2012 at the Wayback Machine. and same English translation, as given on the newsletter of the United States Conference of Catholic Bishops Committee on the Liturgy
- ↑ Letter to the bishops on the occasion of the publication of Summorum Pontificum
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Trento kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |