Darasa
Darasa (kutoka neno la Kiarabu) ni jengo au chumba ambamo mafunzo ya elimu hutolewa, hasa shuleni.
Madarasa hayo hujengwa ili kunapotokea jua, mvua, vumbi au chochote kile ambacho kinaweza kuleta madhara au usumbufu kwa wanafunzi wasipatwe nacho.
Kwa kawaida darasa huwa na ubao wa kufundishia, madawati ya wanafunzi, pia meza ya walimu n.k.
Darasa ni pia jina la mkondo wa wanafunzi wanaosomea humo, na la somo linalofundishwa.
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Darasa kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |